Isaiah 28:1-3

Ole Wa Efraimu


1 aOle kwa lile taji la maua, kiburi cha walevi wa Efraimu,
kwa ua linalosinyaa, uzuri wa utukufu wake,
uliowekwa kwenye kichwa cha bonde lenye rutuba:
kwa ule mji, kiburi cha wale walioshushwa na mvinyo!

2 bTazama, Bwana anaye mmoja aliye na uwezo na nguvu.
Kama dhoruba ya mvua ya mawe na upepo uharibuo,
kama mvua inyeshayo kwa nguvu na mafuriko yashukayo,
atakiangusha chini kwa nguvu.

3 cLile taji la maua, kiburi cha walevi cha Efraimu,
kitakanyagwa chini ya nyayo.
Copyright information for SwhKC